Proverbs 6:6-11


6 aEwe mvivu, mwendee mchwa;
zitafakari njia zake ukapate hekima!

7 Kwa maana yeye hana msimamizi,
wala mwangalizi, au mtawala,

8 blakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi
na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.


9 cEwe mvivu, utalala hata lini?
Utaamka lini kutoka usingizi wako?

10 dBado kulala kidogo, kusinzia kidogo,
bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:

11 ehivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyang’anyi,
na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.

Copyright information for SwhKC